• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya asema juhudi za pamoja zinasaidia kuzuia ugaidi

    (GMT+08:00) 2017-05-04 10:32:57

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema ushirikiano wa karibu kati ya idara za usalama umeisaidia serikali kukomesha uhalifu wa aina mbalimbali, ukiwemo ugaidi.

    Rais Kenyatta ametoa wito kwa idara zote za usalama kuendelea kushirikiana, njia ambayo imesaidia nchi hiyo kugundua na kuharibu mtandao wa magaidi.

    Rais huyo pia amesema, idara za usalama zinatakiwa kuacha wazo kuwa kila idara inafanya kazi kwa kujitegemea, kwa kuwa mtazamo huo umethibitishwa kutokuwa na ufanisi.

    Rais Kenyatta alisema hayo kwenye mahafali ya kikundi cha 19 cha maofisa waandamizi wa jeshi. Maofisa hayo ni pamoja na wakenya na wengine kutoka nchi mbalimbali za Afrika zikiwemo Misri, Nigeria, Zambia, Rwanda, Zimbabwe na Zambia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako