• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya nne ya suala la Syria yafanyika Kazakhstan

    (GMT+08:00) 2017-05-04 10:33:12

    Mazungumzo ya nne kuhusu suala la Syria yamefanyika mjini Astana, Kazakhstan, lakini makundi ya upinzani ya Syria hayakushiriki.

    Ujumbe wa pamoja wa makundi ya upinzani ulithibitisha awali kuwa utahudhuria mkutano huo, lakini habari zinasema ujumbe huo umekataa kushiriki kwenye mazungumzo hayo kutokana na hali ya wasiwasi nchini Syria.

    Habari kutoka kwa ujumbe huo zinasema operesheni za kijeshi mjini Homs na Ladd hazijaisha, na kama hali itatulia, ujumbe wao utashiriki kwenye mazungumzo hayo.

    Wizara ya mambo ya nje ya Kazakhstan imetoa taarifa ikisema makundi ya upinzani ya Syria yamefanya mazungumzo na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Syria na ujumbe wa Marekani, na kwamba ujumbe wao hauna masharti yoyote, na leo utaendelea kushiriki kwenye mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako