• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasisitiza ahadi ya kulinda wanyamapori Afrika

  (GMT+08:00) 2017-05-04 10:33:22

  Ofisa wa China amesema China itaendelea kutoa uungaji mkono kwa ulinzi wa wanyamapori barani Afrika.

  Akizungumza kando ya mkutano wa baraza la Asia na Afrika la sheria za kimataifa AALCO, ofisa wa idara ya usimamizi wa manunuzi na uuzaji wa wanyama na mimea iliyo hatarini Bw. Meng Xianlin amesema, China inaahidi kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na uhalifu dhidi ya wanyamapori.

  Serikali ya China na Kenya zimeandaa mkutano maalum kuhusu mapambano dhidi ya biashara haramu ya wanyama na mimea pori, ukiwa kando ya mkutano wa Baraza la AALCO.

  Kwenye mkutano huo, wizara ya mazingira na maliasili ya Kenya na pande nyingine pia zimemaliza utungaji wa mpango mpya wa hatua ili kuhimiza mapambano dhidi ya biashara haramu za bidhaa za wanyamapori.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako