Rais Vladimir Putin wa Russia amekutana na Kansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel ambaye yuko ziarani nchini Russia. Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, rais Putin amesema, kwenye mkutano wa wakuu wa Kundi la nchi 20 utakaofanyika mwezi Julai nchini Ujerumani, wakuu wa kundi la nchi 20 (G20) watajadili mada mbalimbali ikiwemo namna ya kuondoa vizuizi vya maendeleo ya uchumi wa dunia.
Rais Putina pia amesifu maendeleo ya biashara kati ya Russia na Ujerumani, na kusema biashara kati ya nchi hizo mbili imeanza kuongezeka tangu mwanzo wa mwaka huu, na mustakabali wa uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati yao ni mzuri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |