• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika yajadili masuala ya usalama na ufadhili

    (GMT+08:00) 2017-05-04 18:32:56

    Wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika wameanza mkutano wa siku tatu mjini Kigali, Rwanda hapo jana, ambapo wanajadili masuala ya usalama na utaratibu wa ufadhili.

    Mwenyekiti wa Baraza hilo Mull Sebujja Katende amesema, mkutano huo utajadili njia za kulifanya Baraza hilo kutekeleza majukumu yake vizuri zaidi, pia litajadili utaratibu wa ufadhili wa mipango ya amani na ulinzi, na masuala mengine muhimu yanayohitaji kujadiliwa kwa haraka.

    Amesema nchi zote 15 wanachama wa Baraza hilo zitajadili hali ya usalama katika nchi za Afrika kama vile Somalia, Burundi, Sudan Kusini, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako