• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Morocco kujadili nafasi ya mwanamke katika maendeleo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2017-05-04 18:33:18

    Mkutano wa tatu wa Uwezeshaji wa Wanawake wa Mashariki na Magharibi mwa Afrika umeanza jana mjini Marrakesh, mji mkuu wa Morocco, na unalenga kujadili nafasi muhimu ya wanawake katika maendeleo ya Afrika.

    Mkutano huo wenye kaulimbiu "Nafasi ya wanawake katika uvumbuzi na ubunifu katika viwanda na uchumi na athari zake katika uwezo wa umoja wa Afrika", umewakutanisha wanawake wanaomiliki biashara kutoka mashariki na magharibi mwa Afrika.

    Mkutano huo unatarajiwa kupitisha nyaraka kadhaa zinazohusiana na nafasi ya mwanamke katika kuandaa na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa msingi wa ubunifu na uvumbuzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako