• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Viwavi jeshi waathiri uzalishaji wa chakula

    (GMT+08:00) 2017-05-04 19:03:20

    Kwa mwaka mmoja ujao, itakuwa vigumu kupata chakula cha kutosha baada ya viwavi jeshi kuvamia zaidi ya ekari 8,000 za mahindi katika kaunti ya Trans-Nzoia.

    Viwavi hawa wanahatarishia hazina ya kitaifa ya chakula haswa baada ya sehemu nyingi za nchi kukumbwa na ukame. Uwepo wa viwavi hawa ni kero kwani huenda hali ya njaa ikawa mbaya zaidi mwaka mmoja ujao. Maafisa wa kilimo wakiongozwa na Afisa mkuu wao kutoka kaunti hiyo ambayo inategemewa sana kwa uzalishaji wa chakula cha mahindi nchini, wameanza kusambaza dawa kwa wakulima ili kukabiliana na viwavi hawa.

    Mwezi uliopita serikali ya kaunti hiyo ilitenga shilingi milioni 45 kununua kemikali za kuzuia uenezaji wa viwavi hao. Baraza la magavana na serikali kuu Jumanne zilitangaza bajeti ya shilingi milioni 600 kupambana na wadudu hao kitaifa.

    Kaunti zilizoathirika sana na viwavi hawa ni Bungoma, Trans-Nzoia na kakamega.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako