• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Kenya lazindua sera ya ulinzi kukabiliana na matishio

    (GMT+08:00) 2017-05-05 09:16:30

    Jeshi la Kenya limezindua sera ya ulinzi wa taifa kusaidia kukabiliana na matishio ya kiusalama na kulinda utulivu.

    Jeshi la ulinzi la Kenya (KDF) limesema, sera hiyo itasaidia wanajeshi kuchukua hatua haraka kukabiliana na matisho mbalimbali, kuleta uwiano wa nguvu ambao hauhimizi mashindano ya silaha na nguvu za kijeshi, ambazo pia zina ushawishi kwenye kuzuia matumizi ya nguvu au mabavu wakati wa amani.

    Mnadhimu mkuu wa jeshi la Kenya Jenerali Samson Mwathethe amesema wanaimarisha uwezo wa ugavi wa jeshi, ikiwa ni pamoja na kwenye kupambana na ugaidi na kupunguza madhara ya majanga.

    Sera hiyo pia imesisitiza kuwa mafunzo ya mara kwa mara ni muhimu kwenye kuimarisha uwezo wa jeshi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako