• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zaunda mfuko wa mazingira ili kuhimiza maendeleo endelevu

    (GMT+08:00) 2017-05-05 09:38:57

    Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika zimeunda mfuko wa mazingira ili kuhimiza maendeleo endelevu katika kanda ya Maziwa Makuu barani Afrika.

    Nchi 11 zilizoko bonde la kanda ya maziwa makuu zitanufaika na mfuko huo wa dola laki 5 za kimarekani uliotangazwa kwenye mkutano wa ngazi ya juu uliofanyika katika pwani ya ziwa Victoria.

    Imefahamika kwamba Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Kenya, Malawi, Msumbiji, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania, Zambia na Uganda zitanufaika na Mfuko wa hifadhi ya maziwa makuu barani Afrika.

    Mfuko huo utatumiwa kuunga mkono miradi inayolenga kuboresha maisha na kuimarisha uhifadhi wa mazingira katika kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako