• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waitaka Sudan Kusini kumaliza operesheni za kijeshi katika kanda ya Upper Nile

    (GMT+08:00) 2017-05-05 09:39:21

    Kamishna wa Umoja wa Mataifa masuala ya Haki za Binadamu Bw. Zeid Ra'ad Al Hussein ameitaka serikali ya Sudan Kusini kusimamisha mashambulizi dhidi ya eneo la Aburoc kando ya magharibi ya mto Nile katika jimbo la Upper Nile.

    Bw. Al Hussein pia amezitaka pande mbalimbali zinazohusika na mapambano zifuate sheria za kibinadamu za kimataifa, ikiwemo kuchukua hatua zote kuepusha vifo na majeruhi ya raia.

    Hivi sasa, maelfu ya watu wamekimbilia wilaya ya Aburoc iliyoko kilomita 30 kusini ya Kodoa yenye watu wapatao elfu 50, ambao wengine wanajaribu kuvuka mpaka kuingia Sudan baada ya jeshi la Serikali kutwaa Kodok wiki iliyopita.

    Bw. Al Hussein amesema wakazi wa Aboruc hawana mahali pengine pa kukimbilia, baada ya kundi la SPLA kuzingira sehemu ya kusini, chaguo pekee la kukimbilia upande wa kusini limekuwa hatari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako