• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FKE yalalamikia nyongeza ya mishahara ya asilimia 18

    (GMT+08:00) 2017-05-05 19:04:02

    Shirikisho la waajiri nchini Kenya FKE limelalamikia nyongeza ya mishahara ya asilimia 18 iliyotangazwa na rais Uhuru Kenyatta akisema itawaathiri waajiri wa Kenya. Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Jaqueline Mugo amesema serikali inafaa kupunguza bei ya bidhaa za kimsingi badala ya kuamuru nyongeza ya mishahara. Amesema nyongeza hiyo ya mishahara inaashiria kuwa waajiri watalazimika kuongeza marupurupu mengine ambayo waajiri huwalipa wafanyakazi wao.Marupurupu hayo ni kama vile ya nyumba,matibabu pamoja na hazina ya malipo ya uzeeni NSSF.Kauli hiyo inakuja siku chache tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kuamuru kuwa mishahara ya kiwango cha chini cha wafanyakazi kiongezwe kwa asilimia 18 kama hatua ya kuwakinga dhidi ya kupanda kwa gharama ya maisha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako