• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kuwapa kazi wakandarasi wa ndani

    (GMT+08:00) 2017-05-05 19:04:24

    Serikali ya Tanzania imeahidi kuendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazalendo katika utekelezaji wa miradi mikubwa nchini humo. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa makandarasi ulioandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB mjini Dodoma, makamu wa rais wa nchi hiyo Bi Samia Suluhu Hassan pia amewaonya wale ambao wamekuwa wakitekeleza miradi chini ya viwango vilivyowekwa kwenye mikataba.

    Samia aliagiza kuwa miradi yote ya thamani isiyozidi Sh bilioni 10 wapewe wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani ili wakandarasi hao wasaidie kuongeza ajira kwa vijana wa nchi hiyo na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi.

    Ameongeza kuwa kuwapa miradi mikubwa wakandarasi wa ndani kutasaidia kuwajengea uwezo na kushindana na wakandarasi wa nje hatua ambayo itapelekea fedha nyingi za serikali kubaki ndani ya nchi.Aidha, amewataka wakandarasi hao kukamilisha kazi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. Amesema kuna haja ya wakandarasi hao kujenga uaminifu kwa serikali ili waweze kupewa miradi mikubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako