• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Burundi yatikiswa na ukosefu wa mafuta

    (GMT+08:00) 2017-05-05 19:05:34

    Serikali ya Burundi imesema ukosefu wa fedha za kigeni nchini humo kumesababisha bei ya mafuta kupanda na kuzoretesha uchumi wa nchi hiyo.Kauli hiyo ya serikali inakuja wakati ambapo nchi hiyo imekuwa kwenye msukosuko wa kisiasa kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Katika mji mkuu wa Bujumbura kulikuwa na milolongo mikubwa ya watu kwenye vituo vya kuuza mafuta ya petroli.Wananchi wa Burundi wamesema bidhaa hiyo imekuwa haipatikani katika baadhi ya vituo vya kuuza mafuta. Hatua hiyo imefanya gharama za bidhaa nchini humo kupanda ikiwemo gharama za huduma za usafiri wa teksi. Hali pia inasemekana kuwa mbaya nje ya mji mkuu wa Bujumbura.Wiki jana waziri wa nishati wa Buruyndi Come Manirakiza alinukuliwa akisema tatizo hilo limesababisha na ukosefu wa sarafu za kigeni.Waigizaji bidhaa wameshindwa kuagiza bidhaa kutoka nje kutokana na ukosefu wa dola ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako