• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwakilishi maalumu wa UN na waziri mkuu wa Libya wazungumza kuhusu mchakato wa amani

    (GMT+08:00) 2017-05-05 19:22:47

    Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni mkurugenzi wa ujumbe maalumu unaoshughulikia misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) Bw. Martin Kobler, jana alifanya mazungumzo na waziri mkuu wa serikali ya Umoja ya kitaifa ya Libya Bw. Fayes al-Sarraj kuhusu mchakato wa amani nchini humo.

    Kwenye mazungumzo yao Bw. Kobler amesisitiza umuhimu wa Makubaliano ya siasa nchini Libya katika mchakato wa amani ya nchi hiyo, pia amesema ujumbe maalumu unaoshughulikia misaada wa Umoja wa Mataifa nchini Libya utatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa ajenda ya Makubaliano ya siasa nchini Libya.

    Bw. Sarraj amesema walibya wamekumbwa sana na vita na mfarakano, na sasa ni wakati wa muhimu kutatua mgogoro wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako