• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha kikomunisti na Baraza la serikali la China zapongeza mafanikio ya safari ya kwanza ya ndege aina ya C919

    (GMT+08:00) 2017-05-05 19:33:10

    Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China na Baraza la serikali la China leo zimetuma salamu za pongezi kwa ndege aina ya C919 iliyofanya safari yake ya kwanza kwa mafanikio Kwa mujibu wa salamu hizo, ndege aina ya C919 yenye viti 150 ni ndege ya kwanza ya abiria kutengenezwa na China a na kufuata kiwango cha kimataifa. Mafanikio ya safari yake ya kwanza yanaonesha matokeo makubwa yaliyopatikana katika mradi wa ndege za abiria nchini China, pia ni mnara muhimu wa maendeleo ya viwanda vya ndege za abiria nchini China. Vyombo hivyo vimesema hayo ni mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China inayoongozwa na rais Xi Jinping, na kuonesha umuhimu mkubwa katika kukuza wazo jipya la kujiendeleza, kutekeleza mikakati ya maendeleo kwa njia mpya, kujenga nchi yenye uwezo mkubwa wa kufanya uvumbuzi na uzalishaji, na kuhimiza mageuzi ya kimuundo kwenye utoaji wa bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako