• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (1 Mei-7 Mei)

    (GMT+08:00) 2017-05-05 20:15:44

    Trump afutilia mbali Obamacare

    Rais Donald Trump hatimae amefanikiwa kuifulia mbali mpango wa afya wa Obamacare.

    Mpango huo wa huduma za afya wa Obama ulikuwa ukitoa huduma za bima ya afya kwa mamilioni ya raia wa Marekani kwa nafuu , hivyo kutengua mpango huo ulikua moja ya ahadi ya Trump wakati wa Kampeni za urais.

    Bunge la wawakilishi la Marekani limeupitisha mswada uliobatilisha mpango huu baada ya kupigia kura kwa wengi bungeni.

    Muswada huo umepita kwa ushindi mwembamba wa kura 217 kwa 213.

    Baada ya hapo bunge la Senate litajadili na kutoa maamuzi ya mwisho kuhusiana na mpango huo.

    Mswada huo unatarajiwa kuathiri maelfu ya watu Marekani waliotegemea sana matibabu ya bei nafuu .

    Trump ameseama ana uhakika muswada huo utapita kwenye bunge la Senate.

    Wawakilishi wa chama cha Democrat wameeleza madhara ya kura hii iliyopigwa.

    Raia wa Marekaniu waliandaa maanndamano wakipinga mswada huo.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako