• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuwa mwenyeji wa mkutano kuhusu maendeleo endelevu ya miji

    (GMT+08:00) 2017-05-06 16:55:47

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN-Habitat) limesema maofisa waandamizi kutoka serikali na Umoja wa Mataifa kote duniani watakutana mjini Nariobi kuanzia Jumatatu kujadili njia za kuongeza kasi ya maendeleo endelevu ya miji.

    Wajumbe hao watakaohudhuria kikao cha 26 cha Baraza la Wakurugenzi la UN-Habitat pia watajadili mabadiliko ya hali ya hewa na madhara yake kwa miji.

    Kufuatia Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji uliofanyika mjini Quito mwaka jana, kaulimbiu ya Baraza hilo la Wakurugenzi ni fursa kwa utekelezaji mzuri wa ajenda mpya ya miji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako