• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano ya "maeneo ya kupunguza makali ya mapigano" yaanza kufanya kazi nchini Syria

    (GMT+08:00) 2017-05-06 17:01:13

    Tovuti ya gazeti la al-Watan nchini Syria imesema makubaliano ya maeneo ya kupunguza makali ya mapigano yameanza kufanya kazi nchini humo.

    Kwa mujibu wa makubaliano hayo, serikali na vikosi vya upinzani nchini Syria watasimamisha mapigano kwa miezi sita katika maeneo manne, ambayo ni pamoja na mkoa wa kaskazini magharibi wa Idlib, mkoa wa katikati wa Homs, Ghouta Mashariki iliyo pembezoni mwa mji wa Damascus na maeneo katika mikoa ya Daraa na Qunaitera, kusini mwa Syria. Na maeneo hayo salama au maeneo ya kupunguza makali ya mapigano hayatakuwa na mapigano wala mashambulizi ya anga.

    Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema kabla ya Juni, 4, wasimamizi wa makubaliano hayo wataweka mipaka ya maeneo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako