• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama lalaani shambulizi dhidi ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-05-06 17:51:54

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa likilaani vikali shambulizi dhidi ya tume ya umoja huo nchini Sudan Kusini UNMISS, na kuzihimiza pande mbalimbali nchini humo ziache vitendo vya kimabavu.

    Tarehe 3 usiku, tume ya Umoja wa Mataifa ilishambuliwa na watu wenye silaha katika kambi mjini Leer, jimboni Unity. Askari raia wa Ghana walipambana na washambuliaji mara moja na kuwashinda. Wajumbe wa tume hiyo hawajajeruhiwa wala kuuawa. Na hadi sasa washambuliaji bado hawajathibitishwa.

    Taarifa hiyo inasema mtu yeyote anayeshambulia vikosi vya kulinda amani na watoaji wa msaada wa kibinadamu ataweza kutiwa kwenye orodha ya kuwekewa vikwazo.

    Baraza la Usalama pia limelaani matukio ya kimabavu yanayoendelea kutokea nchini humo, na kuzitaka pande husika kufuata makubaliano yaliyofikiwa ya kusimamisha mapambano, na kuondoa vizuizi kwa utoaji wa msaada wa kibinadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako