• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WFP yatoa mwito kwa jamii ya kimataifa kutoa fedha kusaidia Ethiopia kukabiliana na ukame

    (GMT+08:00) 2017-05-07 17:24:52

    Shirika la Mpango wa Chakula Duniani la Umoja wa Mataifa WFP limetoa mwito kwa jamii ya kimataifa kutoa fedha kwa haraka ili kusaidia Ethiopia kukabiliana na ukame nchini humo.

    Taarifa iliyotolewa na WFP imesema fedha ilizokusanya WFP mwaka huu hazijafikia asilimia 20 ya zinazohitajika, na ni watu milioni moja tu kati ya watu milioni 4.7 waliolengwa walipata msaada wa chakula wa WFP mwezi Aprili. Pia imesema kama fedha za kimataifa zisipotolewa kwa haraka, hali nchini Ethiopia itazorota kwa kasi.

    Serikali ya Ethiopia na wenzi wake wa kibinadamu mwezi Januari walizindua rasmi Waraka wa Mahitaji ya Kibinadamu kwa mwaka 2017, ukitafuta dola za kimarekani 948 ili kuwafikia watu milioni 5.6 wanaohitaji msaada wa haraka wa chakula na usio wa chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako