• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yaidhinisha msaada wa chakula wa dola za kimarekani milioni 50 kwa Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-05-07 17:26:02

    Benki ya Dunia imeidhinisha dola za kimarekani milioni 50 ili kutoa msaada wa chakula wa kupambana na njaa na kuzuia vifo vinavyotokana nayo nchini Sudan Kusini.

    Benki hiyo inasema mradi huo wa dharura wa usalama wa chakula na lishe utanufaisha watu wapatao milioni 4.9 wanaokosa chakula kutokana na mgogoro na ukame nchini humo.

    Fedha hizo pia zitatumiwa kustawisha uzalishaji wa kilimo katika baadhi ya maeneo yanayoathiriwa na ukame.

    Benki ya Dunia itatoa fedha hizo kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP, Shirika la kuhudumia watoto UNICEF na Shirika la Kilimo na Chakula FAO, ambayo yanashughulikia kwa undani usambazaji wa msaada wa dharura nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako