• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Jacob Zuma aingilia kati kukomesha vurugu kwenye miji ya Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2017-05-08 09:10:14

    Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini jana alitembelea mji wa Vuwani kaskazini mwa Afrika Kusini, ambako vurugu zinazoendelea zimekatisha masomo na biashara kwa miezi kadhaa.

    Rais Zuma amekutana na mkuu wa kabila la Vha-Venda Toni Ramabulana na viongozi mbalimbali wadau wa jamii, ikiwa ni pamoja na viongozi wa kanisa, viongozi wa jadi, wafanyabiashara na vijana.

    Vurugu zinazoendelea katika eneo la Vuwani zinatokana na utoaji mbaya wa huduma za jamii kwenye maeneo yenye watu maskini nchini Afrika Kusini. Licha ya kuwa serikali ya Afrika Kusini imepiga hatua kwenye utoaji wa huduma tangu ubaguzi wa rangi ukomeshwe mwaka 1994, bado watu milioni moja wanaishi kwenye mabanda bila umeme, na kutumia mabomba ya maji ya kuchangia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako