• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Algeria yasisitiza ahadi ya kuisaidia Libya kutimiza amani

    (GMT+08:00) 2017-05-08 09:40:15

    Algeria imesisitiza kuwa nchi jirani za Libya zitaendelea na juhudi kuzisaidia pande zinazopambana nchini humo zirudishe amani na kutimiza maafikiano ya kitaifa.

    Baada ya kukutana na mkurugenzi wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya Bw. Martin Kobler, Waziri wa Algeria anayeshughulikia mambo ya Maghreb, Umoja wa nchi za kiarabu na Umoja wa Afrika Bw. Abdelkadar Massahel amesema, makubaliano ya kisiasa yaliyofikiwa mwaka 2015 na pande zinazopambana nchini Libya lazima yawe msingi wa ufumbuzi endelevu wa msukosuko wa Libya.

    Wakati huo huo Bw. Messahel amesema, nchi jirani za Libya zinafanya juhudi kuwasaidia walibya watatue msukosuko, na juhudi hizo hazipaswi kuchukuliwa kuwa uingiliaji katika mambo ya ndani ya Libya.

    Bw. Kobler amesisitiza nafasi muhimu za nchi jirani za Libya katika kurejesha amani na usalama nchini humo. Amesema mkutano wa 11 wa mawaziri wa nchi jirani za Libya ni fursa nzuri ya kuhimiza mchakato wa amani wa Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako