• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria akutana na wasichana 82 walioachiwa huru

    (GMT+08:00) 2017-05-08 09:55:22
    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria jana katika ikulu ya nchi hiyo mjini Abuja alikutana na wasichana 82 wa Chibok walioachiwa huru hivi karibuni.

    Wasichana hao waliachiwa Jumamosi baada ya serikali kuzungumza na wapiganaji wa Boko Haram. Hadi sasa wasichana 105 kati ya wasichana zaidi ya 200 waliotekwa na kundi hilo wameachiwa huru ikiwa ni pamoja na wawili walitoroka wenyewe.

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limekaribisha kurudi kwa wasichana hao na kutaka vyombo husika vya Nigeria kutoa msaada wa kisaikolojia kwa wasichana hao.

    Waziri wa mawasiliano wa Nigeria Bw. Adebayo Shittu ameeleza kuwa anaamini kwamba wasichana wengine waliotekwa wataachiwa haraka kutokana na juhudi za serikali. Rais Buhari ameahidi kufanya kila liwezekanalo kuwaokoa wasichana hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako