• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasema itanufaika na njia ya hariri baharini

    (GMT+08:00) 2017-05-08 10:05:16

    Msemaji wa ikulu ya Kenya Bw. Manoah Esipisu amesema, Kenya iko tayari kunufaika na njia ya hariri baharini, na inatarajia kuwa njia hiyo itafungua maeneo mapya ya maendeleo katika sekta zote za maendeleo ya binadamu.

    Amesema, mpango huo unalenga kuhimiza maendeleo kupitia ushirikiano wa kunufaisha pande zote. Kenya ikiwa ni sehemu ya njia ya Hariri baharini ya karne 21, itanufaika kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuunganishwa kwa mradi wa LAPSSET na njia ya hariri baharini.

    Ameongeza kuwa rais Uhuru Kenyatta wa Kenya atahudhuria mkutano wa baraza la "Ukanda mmoja na Njia moja" utaofanyika Mei 15 mjini Beijing, China pamoja na viongozi 28 wa nchi nyingine duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako