Serikali ya Kenya imetoa tahadhari baada ya kulipuka kwa homa ya dengue katika mji wa Mombasa, huku watu 153 wakithibitishwa kuambukizwa homa hiyo.
Mtendaji mkuu wa afya wa kaunti ya Mombasa Binti Omara amesema, wagonjwa 119 wametambuliwa katika hospitali binafsi kuambukizwa homa hiyo inayoambukiza kupitia mbu, na wengine 34 walithibitishwa katika hospitali za umma katika kaunti hiyo.
Binti Omara amesema, usimamizi umeimarishwa katika maeneo yote baada ya mlipuko wa homa hiyo kuripotiwa huko Kisauni, Jomvu, Changamwe, Nyali, Mvita na Likoni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |