• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bw Macron achaguliwa kuwa rais mpya wa Ufaransa

  (GMT+08:00) 2017-05-08 10:14:14

  Bw Emmanuel Macron mwenye umri wa miaka 39 amechaguliwa kuwa rais mpya wa Ufaransa katika duru ya pili ya uchaguzi iliyofanyika jana.

  Takwimu zilizotolewa na mashirika ya utafiti wa maoni ya raia zimeonyesha kwamba Bw Macron kutoka chama cha mrengo wa kati cha En Marche amepata asilimia zaidi ya 65 ya kura na kufanikiwa kumshinda mpinzani wake Bi Marine Le Pen kutoka chama cha mrengo wa kulia cha National Front. Bw Macron amesema atafanya juhudi zote kuondoa mgawanyiko, na kuihudumia nchi yake kadri awezekavyo katika kipindi chake cha miaka mitano ijayo.

  Serikali ya Ujerumani, waziri mkuu wa Uingereza Bi Theresa May, viongozi wa Umoja wa Ulaya na rais wa Donald Trump wa Marekani wamempongeza Bw Macron kwa ushindi.

  Rais wa sasa Fran├žois Hollande wa Ufaransa atamaliza muda wake wa urais tarehe 14 mwezi huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako