• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia wa Ufaransa aliyeachiwa huru awasili Khartoum, Sudan

    (GMT+08:00) 2017-05-08 18:38:15

    Thierry Frezier, mwanamume raia wa Ufaransa aliyetekwa nyara mwezi Machi mwaka huu mashariki mwa Chad ameachiwa huru na tayari amefika Khartoum, nchini Sudan.

    Mfaransa huyo alionekana kuwa na afya nzuri alipowasili katika uwanja wa ndege wa Khatoum, na ameshukuru juhudi zilizofanywa za kumwokoa.

    Mkurugenzi wa idara ya mipaka na wageni ya wizara ya mambo ya nje ya Sudan Bw. Khalid Al-Kalas amesema idara ya usalama ya Sudan ilifanya uratibu na kubadilishana taarifa za ujasusi na idara za Chad na Ufaransa, na kufanikiwa kuwakamata watekaji nyara na kumwokoa mateka.

    Vyombo vya habari vya Ufaransa vimesema, mateka huyo alifanya kazi katika kampuni moja ya madini, baada ya kutekwa nyara alipelekwa nchini Sudan, ambayo inapakana na Chad.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako