• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ampongeza Macron kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ufaransa

    (GMT+08:00) 2017-05-08 18:39:58

    Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa Bw. Emmanuel Macron kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ufaransa.

    Kwenye salamu zake, rais Xi amesema, Ufaransa ni nchi ya kwanza ya magharibi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China, na uhusiano kati ya nchi hizo una maana ya kimkakati na ushawishi wa kimataifa, na umeendelea kukua katika miaka ya hivi karibuni. Pia amesema zikiwa nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi kubwa duniani, China na Ufaransa zinabeba wajibu muhimu na wa kipekee kwa amani na maendeleo ya dunia, na kwamba maendeleo ya uhusiano kati yao sio tu yanazinufaisha nchi hizo na watu wake, bali pia yatachangia amani, utulivu na ustawi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako