• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaipongeza Marekani kwa kutoa ishara nzuri ya kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kwa njia ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2017-05-08 19:19:20

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema China imeipongeza Marekani kwa kutoa ishara nzuri ya kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kwa njia ya mazungumzo na majadiliano, ambayo inastahili kutumiwa vizuri na pande husika.

    Hivi karibuni, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson alisema Marekani hailengi kubadilisha wala kupindua utawala wa Korea Kaskazini, kuharakisha mchakato wa kuleta muungano wa Korea, na pia kutafuta kisingizio cha kushambulia Korea Kaskazini, bali inataka nchi hiyo kutambua kuwa itapata usalama na ustawi iwapo itasimamisha shughuli zake za nyuklia.

    Bw. Geng amesema China inatoa mwito kwa Marekani kuimarisha mawasiliano na Korea Kaskazini kwenye msingi wa kauli hizo, kutafuta maoni ya pamoja na kujenga hali ya kuaminiana hatua kwa hatua. Pia amesema China inapenda kushirikiana na pande zote husika, na kuendenea kufanya juhudi ili kutatua kiamani suala la nyuklia la Peninsuala ya Korea kwa njia ya mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako