• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • East Africa: Baraza la Mawaziri limesema hakuna kuongezwa kwa bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2017-05-08 19:51:20

    Mawaziri wa kikanda wameamua Bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya 2017/18 itapunguzwa kidogo ikilinganishwa na mwaka wa fedha unaokamilika kutokana na hali ya sasa ya kiuchumi.

    Katika mkutano wa hivi karibuni wa Baraza la Mawaziri mjini Arusha, Tanzania, Katibu Mkuu wa kambi hiyo, Balonzi . Libérat Mfumukeko, aliwasilisha bajeti iliyopendekezwa kwa ajili ya mwaka wa fedha wa 2017/18 ambayo ilifikia kiasi cha dola milioni 113.8 ikilinganishwa na bajeti ya sasa ya dola milioni 101.4.

    Kwa hivyo mawaziri walikubaliana katika Mkutano huo, kwa kuto ongezwa kwa asilimia yeyote katika michango inayotolewa kwa bajeti ya 2017/18.

    Ripoti kutoka kwa Baraza inaonyesha kuwa asilimia 52 sawa na dola milioni 57.3 ya bajeti ijayo ya muungano huo, itatoka kwa rasilimali za ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako