• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magufuli: Kuanzia kesho wahusika Bandari saa 24

    (GMT+08:00) 2017-05-08 19:52:06

    RAIS John Magufuli ameagiza taasisi zote zinazotoa huduma katika Bandari ya Dar es Salaam kuanzia leo ziungane na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kutoa huduma kwa saa 24 ili kukabiliana na tatizo la ucheleweshaji wa mizigo bandarini.

    Alitoa agizo hilo, wakati alipokuwa akizindua Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kuongoza Mkutano wa 10 wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu, Dar es Salaam.

    Hata hivyo, Rais Magufuli aliwataka wafanyabiashara na wawekezaji wajirekebishe kwa kasoro ambazo baadhi yao wanazo ikiwemo ukwepaji wa kodi, kupandisha viwango vya bei kwa huduma wanazotoa serikalini, kujihusisha na rushwa, kutaka faida kubwa bila kuwajali wananchi na kutochangamkia fursa za uwekezaji wa ndani na nje ya nchi licha ya juhudi zake za kuwaleta viongozi na wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako