• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda mpango mpya wa AfDB ya kusaidia vijana zaidi ya 200 kushiriki katika kilimo biashara

    (GMT+08:00) 2017-05-08 19:52:22

    Wadau wa ndani katika sekta ya kilimo nchini Rwanda, wamekaribisha mpango mpya wa benki ya Afrika ya Maendeleo ya Benki ya (AfDB) kusaidia vijana kushiriki katika shughuli za kilimo.

    Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imesema mpango huu wa miaka mitano unania ya kusaidia vijana zaidi ya 200 kushiriki katika kilimo biashara katika bara la Afrika.

    Mpango huu ulitangazwa katika hivi karibuni katika mkutano wa kilimo biashara wa vijana Ibadan, Nigeria.

    Zaidi ya asilima 72 ya idadi ya watu wa Rwanda wameajiriwa katika sekta ya kilimo, na kilimo ni moja ya mchangia mkubwa wa uchumi wa taifa.

    Tayari wakulima wa ndani wamekubali mpango huo, na wanaimani mpango huo utasaidia katika kubadilisha sekta ya kilimo nchini Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako