• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Kenya yaahidi kupunguza bei za bidhaa

  (GMT+08:00) 2017-05-09 09:10:38

  Bunge la Kenya linatarajiwa kufanya kikao maalum leo kujadili njia za kupunguza gharama za maisha wakati huu bei ya unga, sukari na maziwa nchini humo ikiendelea kupanda.

  Wakaazi wengi wanaolipwa chini ya dola tatu kwa siku wanaona kwamba maisha yamekuwa magumu na hivyo wanatoa wito kwa serikali kuingilia kati.

  Ronald Mutie anaripoti kutoka Nairobi.

  Ndio tetesi za kila siku kwa wakaazi wa miji na vijiji nchini Kenya.

  Lalama za kupanda kwa bei ya unga, maziwa na bidhaa nyingine za matumizi ya kila siku.

  Kilio kimefika kwenye meza ya serikali.

  "Ghamara ya unga imeenda juu na sisi twafanya juu chini ili kusaidia mwananchi wa kawaida " anasema rais Uhuru Kenyatta.

  Sasa bei ya maziwa kwa nusu lita ni dola 0.6 sawa na shilingi 65 kutoka ile ya 42 unga kilo mbili imepanda kutoka dola moja hadi dola 1.5 huku hayo sukari kilo moja ikiwa ni dola mbili kutoka bei ya siku chache zilizopita ya dola 1.5.

  Na kwa raia wengi wenye mapato ya chini inakuwa vigumu kula mara tatu kwa siku.

  "Ningeomba rais arejeshe chini bei za biadhaa za kimsingi. Zamani ukiwa na shilingi hamsini ungenunua vitu nyingi na ukule kwa nyumba lakini sasa bei ya unga imeenda juu"anasema Bernard mkaazi wa Nairobi

  Kinacholaumiwa kwa kupanda kwa bei ya vyakula ni ukame ulioadhiri uzalishaji kwenye maeneo kadhaa nchini Kenya.

  Uhaba wa nafaka umepelekea wafanyabiashara kuvuka mipaka kununua kutoka nchi jirani.

  Katika kaunti ya Migori kwa mfano, wafanyabiashara wamekuwa wakisafiri hadi Tanzania kununua mahindi yanayouzwa kwa bei nafuu.

  Bidhaa nyingine zinazonunuliwa kutoka Tanzania ni mchele, bidhaa za urembo na dawa ya meno.

  Lakini kuna afueni, kuanzia jumanne hii bunge linaandaa kikao maalum ili kujadili kutengwa kwa bajeti ya ziada itakayo walinda wakenya dhidi ya gharama ya juu ya maisha.

  Rais Uhuru Kenyatta anasema

  "Tumeuliza spika aitishe bunge, wabunge warudi ili tuone ni nini tunaweza kufanya kwa bajeti, ndio tuweze kupoesha ile shida wananchi wako nayo wakati huu, tushukishe hii bei ya unga, ndio watu waweze kuwa na na nafuu wakati tukitafuta suluhu ya muda mrefu"

  Na mwezi mmoja uliopita serikali ilitenga dola milioni 7 kwa kampuni ya maziwa KCC ili kusaidia kurejesha chini bei ya bidhaa hiyo.

  Naibu wa rais wa Kenya William Ruto akitembelea kiwanda cha KCC cha Eldoret wakati huo alisema pia serikali iko na mipango ya kuweka mitambo ya kisasa kwenye viwanda vyote nchini ili kuwezesha uhifadhi wa maziwa ili kutumika wakati wa kiangazi na hivyo bei kusalia chini.

  "Kama kuna mkulima anasema hawezi kusubiri mwezi mmoja basi anaweza kulipwa ndani ya wiki mbili ama hata wiki moja ili tuondoe tatizo la wachuuzi kwa biashara ya maziwa"

  Mvua nchini Kenya zimeanza kunyesha lakini mavuno yanatarajiwa baadaye mwezi julai, na hadi hapo serikali itajukumika kutafuta mbinu tofauti za kurejesha chini gharama za maisha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako