• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan na Sudan Kusini kufanya mkutano dharura kuhusu masuala yaliyopo kati yao

    (GMT+08:00) 2017-05-09 09:29:08

    Vyombo vya habari vya Sudan vimesema, Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana kufanya mkutano wa dharura jumapili ijayo huko Addis Ababa, ili kujadili masuala ambayo bado hayajatatuliwa kati yao.

    Mkurugenzi wa ofisi ya mawasiliano ya Umoja wa Afrika Bw. Mahmoud Kan amesema, nchi hizo mbili zitafanya mkutano tarehe 14 hadi 15 mwezi Mei, chini ya uangalizi wa jopo la ngazi ya juu la Umoja wa Afrika AUHIP, ambapo zitajadili eneo salama lisilo na shughuli za kijeshi, "mstari wa Sifuri" na makubaliano mengine.

    Habari nyingine zimesema mkurugenzi wa shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Bibi Leila Pakkala amesema, zaidi ya watoto milioni moja, wakiwa asilimia 62 ya wakimbizi milioni 1.8 kutoka Sudan Kusini, wamekimbia mgogoro nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako