• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazitaka nchi za Afrika kutumia mtandao wa posta kuimarisha utumaji wa fedha

    (GMT+08:00) 2017-05-09 10:00:10

    Kenya imetoa mwito kwa nchi za Afrika kutumia mtandao mkubwa wa posta kuimarisha upatikanaji wa fedha katika nchi za Afrika.

    Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano wa 36 Umoja wa Posta Afrika Waziri wa teknolojia ya habari na mawasiliano wa Kenya Bw Joe Mucheru amesema, mtandao wa Posta una mazingira mazuri ya kuwasaidia kwenye mambo ya fedha wanawake, watu maskini, wenye elimu ndogo na wale walioko kwenye sekta isiyo rasmi.

    Kwa mujibu wa Umoja wa Posta duniani UPU, mwaka jana watu bilioni mbili duniani walikuwa hawana njia ya kupata huduma za kifedha.

    Mwenyekiti wa mamlaka ya mawasiliano ya Kenya Bw Ngene Gituku amewataka wasimamizi wa posta barani Afrika kuchukua hatua kuendeleza mtandao wa posta uliopo ili utumike kwenye biashara ya matandao wa internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako