• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN-Habitat latoa dola milioni 11 kuboresha makazi duni

    (GMT+08:00) 2017-05-09 10:05:12

    Shirika la Mpango wa Makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat limetoa dola milioni 11 za Kimarekani ili kusaidia miradi ya kuboresha makazi duni katika nchi za Afrika, Caribbean na Pasifik.

    Maofisa wamesema Kamati ya Ulaya itatoa pesa ambazo zitaingizwa kwenye duru ya tatu ya Mpango huo kuanzia mwaka 2017 hadi 2021. Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Habitat Aisa Kirabo Kacyira amesema fedha hizo zitawezesha upatikanaji wa nyumba bora mijini, kwa ajili ya watu maskini katika nchi hizo.

    Habitat itatekeleza duru ya tatu ya kuboresha makazi duni ya nchi shiriki. Mradi huo wa miaka minne unahusu kujenga uwezo, kuundwa kwa sera na kubadilishana ujuzi ili kuboresha miji katika nchi zinazoendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako