• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Senegal wakutana na makamu wa rais wa China

    (GMT+08:00) 2017-05-09 10:24:26

    Makamu wa rais wa China Li Yuanchao ambaye yuko ziarani nchini Senegal amekutana na kufanya mazungumzo na Rais na waziri mkuu wa nchi hiyo mjini Dakar.

    Alipokutana na Rais Sall Bw Li Yuanchao amesema ziara yake nchini Senegal ina lengo la kutekeleza makubaliano ya ushirikiano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Johannesburg wa Baraza la ushirikiano wa China na Afrika. Amesema China inapenda kudumisha mawasiliano na Senegal na kuimarisha ushirikiano katika masuala ya amani na usalama, na mambo ya kimataifa.

    Kwa upande wake Rais Macky Sall amesema Senegal siku zote inaichukulia China kama mwenzi muhimu wa ushirikiano, inashikilia sera ya kuwepo kwa China Moja, inaunga mkono msimamo wa China kuhusu suala la Bahari ya Kusini ya China, na pia inatilia maanani mapendekezo ya Ukanda Mmoja na Njia Moja.

    Alipokutana na Waziri mkuu wa Senegal Bw Mahammed Abdallah Dionne, Bw Li amesema China inauunga mkono ujenzi wa miundombinu nchini Senegal na kupenda kuimarisha ushirikiano kwenye sekta za raslimali watu, kilimo na viwanda. Bw Dionne amesema kuwa nchi yake inaikaribisha China kuwekeza nchini Senegal.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako