Mashuhuda wamesema gari moja lililokuwa na mabomu liligongeshwa kwenye mgahawa huo ulioko karibu na Ofisi ya Uhamiaji, ambao wateja wake wengi ni wafanyabiashara, wabunge na maofisa wa serikali.
Shambulizi hilo lilitokea saa chache tu baaada ya rais Mohamed Abdullahi Farmajo kutembelea sehemu ya Lower Shabelle inayodhibitiwa na kundi la Al-Shabaab. Kundi hilo limetangaza kuhusika na shambulizi hilo, na kusema liliwalenga maofisa wa jeshi, idara ya uhamiaji na washauri wa serikali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |