Bw. Chediek amesema kongamano la ushirikiano wa kimataifa la Ukanda Mmoja na Njia Moja litakalofanyika tarehe 14 hadi 15 Mei hapa Beijing, lina uhusiano mkubwa na ushirikiano wa nchi za Kusini-Kusini, na litahimiza zaidi ushirikiano huo.
Pia amesema pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lililotolewa mwaka 2013 litasaidia kuongeza ushirikiano kati ya nchi mbalimbali zinazoendelea, kuchangia maendeleo ya uchumi na ujenzi wa miundombinu katika nchi zinazojumuishwa na pendekezo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |