• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ugonjwa wa ajabu uliozuka nchini Liberia huenda ni homa ya uti wa mgongo

    (GMT+08:00) 2017-05-09 18:34:56

    Waziri wa afya wa Liberia Bernice Dahn amesema, ugonjwa wa ajabu uliozuka kusini mashariki mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita unahisiwa kuwa ni homa ya uti wa mgongo.

    Akiongea na waandishi wa habari mjini Monrovia, waziri Dahn amesema kuwa, damu ya waathirika iliyopimwa kwenye maabara imethibitisha kuwa nchi hiyo inakabiliwa na uwezekano wa mlipuko wa ugonjwa wa uti wa mgongo. Amesema ugonjwa huo ulianza katika mji wa Greenville, mji mkuu wa kaunti ya Sinoe, na umesambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo katika wiki mbili zilizopita, ambapo jumla ya kesi 31, ikiwemo vifo 13 vimeripotiwa mpaka sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako