Shilingi ya Uganda imeonyesha hatua za kuanza kustawi dhidi ya dola ya Marekani katika soko la hisa wiki hii.
Siku ya jumatatu na jumanne,dola moja ya Marekani iliuzwa kwa shilingi 3625 hadi 35 .
Kwa mujibu wa benki kuu ya Uganda ,sarafu za kimataifa haswa dola zimepoteza thamani kiasi kidogo mwezi huu kutokana na athari chanya za uchumi wao.
Pauni ya Uingereza aidha ilishuka pia wiki hii.
Upande wa bidhaa hali ilikuwa tofauti kwani bei ya tango ama malenge imeshuka vile vile wiki hii ijapokuwa ile ya tikiti maji iliopngezeka.
Jijini Kampala hali ya kupanda kwa bei ya vyakula imeshuhudiwa kama miji mengine ya nchi za Afrika Mashariki.
Malenge yanauzwa kwa shilingi 3500 kutoka 2000 nayo mananansi yameshuka kutoka 2500 hadi 2000.
Hii ni baada ya mvua kuanza kunyesha katika sehemu nyingi nchini Uganda.
Wataalamu wa masuala ya uchumi wametoa mwito kwa waganda kuregelea kilimo cha chakula chao na biashara ili kupunguza makali ya bei ya juu ya vyakula na gharama ya maisha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |