• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi ya mpira wa kikapu ya NBA, Washington Wizards waifunga Boston Celtics

  (GMT+08:00) 2017-05-10 09:19:10

  Wakiwa nyuma kwa kupoteza michezo 2 mfululizo, Washington Wizards wamerejea nyumbani na kuwafunga Boston Celtics 121 kwa 102, Wakiongozwa na mchezaji anayeonekana kuimarika kila kukicha John Wall.

  Wizards walinufaika kwa kupata pointi 34 kutokana na Celtics kupoteza mipira kirahisi, Washington walifanikiwa kuipoteza Celtics kwa kufunga mfululizo pointi 26-0 kuelekea katika robo ya 3.

  Mchezaji wa Washington, John Wall alikuwa na pointi 27 na pasi na kuwatesa Celtics ambapo katika michezo ya mtoano ameweza kufunga walau pointi 20 na kutoa pasi zaidi ya 7 katika michezo 10 ya mtoano mfululizo, akiwa mchezaji wa kwanza tangu Michael Jordan. Mchezaji Bradley Beal yeye alifunga alama 29 points.

  Isaiah Thomas ambaye alikuwa na pointi 17 katika dakika 15 za mwanzo alikabwa vyema na kumaliza mchezo akiwa na alama 19 tu kwa upande wa Boston Celtics.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako