• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanajeshi sita wa Somalia wameuawa kwenye mlipuko wa mabomu ya ardhini

    (GMT+08:00) 2017-05-10 09:32:24

    Askari sita wa Somalia wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mlipuko wa mabomu ya kutegwa ardhini uliotokea jana mkoani Bay nchini Somalia.

    Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo waziri wa habari wa Jimbo la Kusini Magharibi, Ugaas Hassan amesema wanajeshi hao waliuawa baada ya gari lao kukanyaga bomu wakati wakikimbilia kutoa msaada kwa vikosi vya mkoa vinavyopambana vikali na kundi la Al-Shabaab. Amesema magari mengine mawili ya askari hao yametekwa na kundi hilo na baadhi ya askari pia hawajulikani walipo.

    Mashuhuda wamesema takriban watu wanane wameuawa baada ya wapiganaji kuutwaa mji muhimu wa Goofgaduud karibu na mji wa Baidoa baada ya vita kali na askari wa kusini magharibi na serikali ya Somalia.

    Shambulizi hilo limetokea saa chache tu baada ya rais wa Somalia Mohamed Abdulahi Farmajo kutembelea mji wa Afgoye uliopo katika jimbo la Kusini Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako