• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Walinzi wanne wa amani wa UM nchini Afrika ya Kati wauawa katika shambulizi

    (GMT+08:00) 2017-05-10 09:41:13

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, askari wanne wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afrika ya Kati wameuawa na wengine nane kujeruhiwa baada ya msafari wa magari yao kushambuliwa usiku wa jumatatu na wapiganaji wasiojulikana karibu na mji wa kusini wa Bangassou.

    Bw. Dujarric amesema, wapiganaji wanane wa kundi la Anti-Balaka pia waliuawa kwenye mapambano hayo.

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umelaani shambulizi hilo, na kusisitiza kuwa vitendo vya kuwaua na kuwajeruhi walinzi wa amani vinachukuliwa kuwa ni uhalifu wa kivita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako