• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani aidhinisha kutoa silaha kwa kundi la Kikurdi nchini Syria

    (GMT+08:00) 2017-05-10 19:53:05

    Ikulu ya Marekani imethibitisha kwamba, rais Donald Trump wa nchi hiyo ameidhinisha wizara ya ulinzi kutoa silaha kwa kundi la Kikurdi linaloshiriki kwenye mapambano dhidi ya kundi la IS nchini Syria.

    Msemaji wa ikulu ya Marekani Sean Spicer amesema, hatua hiyo inalenga kuhakikisha wapiganaji wa Kikurdi wa vikosi vya SDF vya Syria wanapata ushindi bila tatizo katika mapambano dhidi ya IS huko al-Raqqa nchini Syria, wakisaidiwa na mashambulizi ya anga ya muungano wa kimataifa wa majeshi unaoongozwa na Marekani.

    Ameongeza kuwa Marekani inafahamu wasiwasi wa kiusalama wa mshirika wake Uturuki, nchi inayowachukulia wapiganaji wa Kikurdi kama magaidi, na itajitahidi kuzuia hatari za usalama zitakazoweza kutoka kwa kulipatia kundi hilo silaha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako