• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Inter Milan yakataa kuzungumzia taarifa za kumtaka ea Antonio Conte ajiunge nao

    (GMT+08:00) 2017-05-11 08:42:19

    Klabu ya Inter Milan ya Italia imekataa kuzungumzia taarifa kwamba inapanga kuwasilisha ombi kumtaka meneja wa Chelsea Antonio Conte ajiunge nao. Inter wamemtimua kazi meneja wao Stefano Pioli.

    Taarifa nchini Italia zinasema klabu hiyo ya Serie A, inapanga kumuahidi Conte ujira wa £250,000 kwa wiki iwapo ataondoka Chelsea, klabu ambayo ameiongoza kwa msimu mmoja pekee.

    Pioli alifukuzwa kazi Jumanne miezi sita tu baada ya kuteuliwa kuwa mkufunzi mkuu. Mkufunzi huyo mwenye miaka 51 alijaza nafasi ya Frank de Boer mwezi Novemba na alitia saini mkataba wa kuwa meneja hadi Juni 2018.

    Conte, mwenye miaka 47, ambaye alikuwa meneja wa timu ya taifa ya Italia, alihudumu kama meneja wa mahasimu wakuu wa Inter, Juventus kati ya 2011 na 2014. Inter, wakiwa wamesalia na mechi tatu za kucheza msimu huu, wapo nafasi ya saba Serie A, alama tatu nyuma ya AC Milan ambao wanashikilia nafasi ya mwisho ya kufuzu kwa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.

    Inte Milan hawajashinda mechi hata moja katika mechi saba walizocheza karibuni ligini. Mkufunzi wa timu ya vijana Stefano Vecchi amepewa majukumu ya kuongoza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako