• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wairaq 622,000 wakimbia operesheni za kijeshi Mosul

    (GMT+08:00) 2017-05-11 09:19:15
    Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema watu takriban 622,000 wamekimbia makazi yao huko Mosul, kaskazini mwa Iraq kutokana na operesheni zinazofanywa na jeshi la serikali dhidi ya kundi la IS mjini humo.

    Operesheni hizo zilizoanza mwezi wa Oktoba mwaka jana zimepata maendeleo na kukomboa sehemu za mashariki mwa Mosul kutoka kwa kundi la IS.

    Habari zinasema juzi serikali ilifungua tena daraja la Nimrud. lililofungwa tangu tarehe 2 mwezi wa Mei kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji na kukwamisha usafirishaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako