• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Rwanda azitaka nchi za Afrika kufanya kazi pamoja kuhakikisha zinapata teknolojia

    (GMT+08:00) 2017-05-11 09:28:09

    Rais Paul Kagame wa Rwanda ametoa mwito kwa nchi za Afrika kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha watu wao wanaweza kutumia teknolojia mbalimbali.

    Akiongea mjini Kigali kwenye mkutano wa Transform Afrika 2017, Rais Kagame amesema teknolojia ni nyenzo yenye nguvu, inayoweza kuwaleta pamoja wadau mbalimbali kutambua changamoto na kuzitafutia suluhisho.

    Rais Kagame pia amesema kama teknolojia inatenganisha watu, basi itakuwa inatumika kwa makosa. Amekumbusha kuwa kama wanawake na wasichana wanaachwa kwenye matumizi ya teknolojia, basi kazi inatakiwa kufanyika ili kuondoa pengo hilo na sio kulikuza.

    Mkutano huo wa Kigali unawakutanisha Rais wa Rwanda, mameya wa miji mbalimbali ya Afrika, na maofisa wa Tehama kutoka nchi mbalimbali wanaohusika na sekta za uchumi wa kidigitali, miundombinu, fedha, afya, elimu na nishati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako