• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki yaihimiza Marekani kuacha kulipatia silaha Kundi la Kikurdi la PKK

    (GMT+08:00) 2017-05-11 09:39:54
    Rais Recep Erdogan wa Uturuki ameitaka Marekani iache kulipatia silaha tawi la Chama cha wafanyakazi cha Kikurdi PKK nchini Syria kabla ya kuanza ziara yake nchini Marekani wiki ijayo.

    Rais Erdogan amesema kundi moja la kigaidi haliwezi kutokomezwa na kundi jingine, na kwamba lolote linalotokea nchini Syria na Iraq lina uhusiano na usalama wa Uturuki. Amesema ataeleza wasiwasi huo atakapokutana na rais Donald Trump tarehe 16 mwezi huu, na kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa NATO utakaofanyika tarehe 25 mjini Brussels.

    Waziri wa ulinzi na usalama wa Uturiki Bw Fikri Isik amesema uamuzi wa Marekani wa kuwapatia silaha waasi wa Kikurdi nchini Syria hauna manufaa kwa Marekani wala kanda hiyo.

    Habari zimesema vikosi vya SDF vya Syria, vinavyoongozwa na kundi la kikurd YPG na kuungwa mkono na muungano wa kimataifa wa kupambana na kundi la IS, jana vilikomboa bwawa la Euphrates na mji wa Tabqa kutoka kwa Kundi la IS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako